HIKI NDICHO KILICHOMUUWA EPHRAIM KIBONDE MTANGAZAJI WA CLOUDS RADIO
Leo March 7, 2019 Habari kubwa Tanzania ni kifo cha Mtangazaji wa Clouds FM Ephraim Kibonde kilichotokea Mkoani Mwanza na kuthibitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Tukiwa bado na majeraha mabichi ya msiba wa Mkurugenzi wetu wa Vipindi na Uzalishaji #RugeMutahaba, kwa masikitiko makubwa tunatangaza kifo cha aliyekuwa Mtangazaji wa kipindi cha jahazi kinacholushwa saa kumi alasiri hadi kumi na mbili jioni kupitia radio ya clouds#EphraimKibonde kilichotokea alfajiri ya leo (Machi 7 2019)
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza amethibitisha kwamba Mtangazaji wa CloudsFM Ephraim Kibonde amefariki akiwa Mwanza, alianza kusumbuliwa na Presha toka Bukoba kwenye msiba wa Ruge Mutahaba na kuhamishiwa Mwanza. Pia Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dr. Thomas Rutachunzibwa katika taarifa yake, amesema Mtangazaji wa CloudsFM #EphraimKibonde alifariki akiwa njiani kuhamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Mwanza akitokea Hospitali ya Uhuru.
Utakumbuka Kibonde ndiye aliyeongoza ratiba ya msiba wa ruge mutahaba kama MC (mshereheshaji) katika shughuli za mazishi ya Ruge.kuanzia siku ya kwanza ya airport,kuupokea mwili wa ruge office za clouds ,kuuaga mwili viwanja vya kalimu gee.
Kibonde ni baba wa watoto watatu (Junior, Hilda na Illaria ).Pia alizika mke wake mwaka jana.moja ya hadithi ambayo kibonde aliwaambia wenzake wakati wa msiba ni jinsi ambavyo yeye na mkewe waliwahi kujadili juu ya maisha ya watoto wao siku wakiondoka. Waliamini mmoja akiondoka, mwingine atawalea.
Leo wamekwenda wote: Junior, Hilda na Illaria (watoto watatu wa Kibonde), Mungu atawafuta machozi, yeye ajua yote.
Ukipitia katika Instargram akaunti ya Ephraim Kibonde utakuta kitu cha mwisho kukipost ni picha ya Mke wake kipenzi ambaye nae amefariki na kuzikwa kinondoni jijini dar es salaam. Hapo utafahamu jinsi gani kibonde alivyompenda mke wake kipenzi.kwetu sisi tunaamini kwa sasa kibonde amekutana na mke wake na wapo kwenye amani ya milele na wameachana na dunia hii yenye kila aina ya matatizo.
Tunamtukuza Mungu kwa Maisha ya Kibonde, na kumuomba yeye ampokee na kumpuzisha katika makao ya amani ya milele.Pia awape Mungu awape nguvu ,amani na subira familia ya mpendwa wetu kibonde.
Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi kuhusiana na msiba huu. Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa, Jina lake Lihimidiwe. #RIPKibonde #Pumzikakwaamani