jinsi ya kupata loss repoprt ya police kwa haraka kwa njia ya mtandao - ulimwengu wa teknolojia

Breaking

About Me

Peoples Solution

Sunday 12 January 2020

jinsi ya kupata loss repoprt ya police kwa haraka kwa njia ya mtandao

Loss report sasa kupatikana kwa njia ya mtandao



Jeshi la Polisi nchini kupitia kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), kwa kushirikiana na Government e-Payment Gateway (GePG), limeanzisha mfumo wa upatikanaji wa fomu ya upotevu (Police Loss Report), kupitia mtandao wa https://Lormis.tpf.go.tz na kufanya malipo kwa njia ya simu kwa mfumo wa GePG.

Mfumo huo ulianzishwa mwezi Machi, 2019 na kitengo cha TEHAMA Makao Makuu ya Polisi, kwa lengo la kupunguza gharama na kurahisisha upatikanaji wake katika vituo vya Polisi, kwa sasa mfumo unafanya kzi nchi nzima humuwezesha mtu yeyote kufanya maombi na malipo ya Loss Report kwa njia ya mtandao na baadaye mwombaji kwenda Kituo cha Polisi ili kukamilisha huduma hiyo.
kama umepoteza kitu na unaitaji  loss report form (fomu ya taarifa ya kupotelewa kitu) ya police  tembelea tovuti  https://lormis.tpf.go.tz/

Mwombaji wa fomu ya upotevu kwa njia ya mtandao, atatakiwa kufuata hatua zifuatazo:-

HATUA MUHIMU
1. Jaza hiyo form kupitia mtandao kwa kutoa maelezo ya upotevu.




Akisha jaza fomu hiyo atapatiwa ‘control number’.

2. Utapata Control Number 99XXXXXXXXXX
Baada ya kupatiwa ‘control’ namba atalipia Tsh 500/= kwa njia ya mtandao.

3. Lipa Tsh 500/= kwa njia ya mtandao

4. Nenda kituo chochote cha polisi kwa ajili ya uthibitisho
Baada ya kufanya malipo atatakiwa kwenda kituo chochote cha Polisi kwa ajili ya
uthibitisho.

5. Print barua yako kwa wakati wako.
Baada ya kukamilisha hatua zote mwombaji ataprinti fomu hiyo kwa wakati wake.

Jeshi la Polisi nchini linatoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano katika mapambano dhidi ya uhalifu kwa kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu ili kuendelea kudumisha amani na usalama wa nchi.

Tafadhari tuwajulishe wananchi kila tunapopata fursa ya kukutana nao awe mmoja au wengi.

LIPIA BARUA YA UPOTEVU (LOST REPORT) KUPITIA SIMU YAKO