Dar es salaam: Mfanya biashara mkubwa Tanzania na afrika Said Salim Bakhresa .Atangaza kuanzisha kampuni ya simu yenye kasi ya ajabu na ubora wa ali ya juu.Hii ni baada ya kufanikiwa kwa kiasi kikubwa ndani ya sekta ya biashara ya kuzambaza bidhaa za vinywaji na vyakula na baadae kufungua kampuni ya Azam media ambayo inamiliki TV na ving'amuzi vya Azam.
Mkurugezi na Mmiliki wa kampuni ya Bakhresa Group of Companies Said Salim Bakhresa ametangaza kuanzisha kampuni ya mawasiliano ya Azam mobile network itakaofanya kazi ndani ya Tanzania.
Akiongea na Gazeti la The Citizen Mkurugenzi wa Bakhresa Group Corporate Hussein Sufian Ally amesema kuwa mtandao huo wa simu utazinduliwa miezi michache ijayo kuanzia hivi leo(jana) na kusema kuwa mtandao huo unakusudiwa kutoa huduma kwa gharama nafuu kwa watanzania, na usikivu mzuri wa mawasiliano kwa watumiaji wake.
Aidha Sufian amesema kuwa mtandao huo utakuwa na kasi ya Internet ya hali ya juu yenye 4G, na pia wamejipanga kutumia teknolojia ya kisasa inayotumika ulimwenguni kwa sasa ili kuendana na mahitaji ya soko.
JE WEWE UNAFIKI AZAM WATAFANIKIWA KULETA MABADILIKO YA HALI YA JUU KWENYE SEKTA YA MAWASILIANO UKITOFANANISHA NA MITANDAO TULIYO NAYO SASA.
JE WEWE UNAFIKI AZAM WATAFANIKIWA KULETA MABADILIKO YA HALI YA JUU KWENYE SEKTA YA MAWASILIANO UKITOFANANISHA NA MITANDAO TULIYO NAYO SASA.
Ungana Nasi Kwenye Mitandao ya Kijamii
KALIBU KWENYE GROUP NA PAGE YETU YA FACEBOOK KWA JINA LA ULIMWENGU WA TEKNOLOJIA.WHATSAPP KWA NAMBA 0653270429
KALIBU KWENYE GROUP NA PAGE YETU YA FACEBOOK KWA JINA LA ULIMWENGU WA TEKNOLOJIA.WHATSAPP KWA NAMBA 0653270429
Ulimwengu wa teknolojia Sisi ni suluhisho lako namba moja katika masuala yote ya Teknolojia,ya TEHAMA TANZANIA tembelea Kila Siku.