TANZANIA YAANZA KUTENGENEZA SIMU JANJA ZAKE(SMART PHONE) KUPITIA KAMPUNI YA IPP TOUCHMATE INAYOMILIKIWA NA MENGI - ulimwengu wa teknolojia

Breaking

About Me

Peoples Solution

Saturday 3 November 2018

TANZANIA YAANZA KUTENGENEZA SIMU JANJA ZAKE(SMART PHONE) KUPITIA KAMPUNI YA IPP TOUCHMATE INAYOMILIKIWA NA MENGI



TANZANIA YAANZA KUTENGENEZA SIMU ZAKE YENYEWE.KUPITIA KAMPUNI YA IPP TOUCHMATE MOBILE.

                                              
Kampuni ya IPP  chini ya mkurugenzi mtendaji wake bwana Reginald Mengi.Hivi leo imetangaza kuanza ujenzi wa kiwanda cha kwanza cha kutengeneza simu janja maarufu kama smartphone, Ndani ya Tanzania.Simu hizo zitakuwa na uwezo wa kukaa na chaji kwa muda wa wiki moja na kwa wasiokuwa na umeme wanaweza chaji kwa nguvu ya Jua. 

Hayo yamejiri wakati bado tukisubiri kuanza kwa ujenzi wa kiwanda cha simu.Ambacho serikali waliahidi kuanza kwa kutengenezakiwanda hiko   huko visiwani zanzibar.

IPP TouchMate ndiyo jina la kampuni hiyo ambayo ilizinduliwa na ndugu Reginald Mengi.Kampuni itajihusisha na utengenezaji mbalimbali wa vifaa vya kielectroniki kama vile simu za mikononi ,Tableti,Saa janja na Laptop


Kiwanda hicho kitakachokuwa cha kwanza nchini na Afrika Mashariki, kitajengwa eneo la Mikocheni jijini Dar es salaam, ambapo uwekezaji wake ukikadiriwa kuwa ni shilingi bilioni 11 na kitaanza uzalishaji ndani ya miezi 3 ijayo, kikitarajia kuajiri takribani watu elfu mbili kwa awamu ya kwanza.

Akizungumza na wanahabari Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP Dkt. Reginald Mengi amesema kiwanda hicho kitakuwa na mchango mkubwa kwenye uchumi na sehemu kubwa ya watakaoajiriwa ni watu wenye ulemavu.

                           

"Simu zitakazotengenezwa na IPP TouchMate zitakuwa na uwezo wa kukaa na chaji kwa muda wa wiki moja na lengo litakuwa ni kuendana na mazingira ya maisha halisi ya Tanzania", amesema Dkt. Mengi.

Pamoja na hayo kwa mara ya kwanza kampuni ya TouchMate ilizindua simu yake ihitwayo TouchMate 4GX1 ambayo ilisifiwa kama simu ngumu zaidi na yenye kudumu na chaji kwa muda wa wiki moja

Tayari ufungaji mitambo kwenye kiwanda hicho kitakachojulikana kama IPP TouchMate umeshaanza ambapo mbali ya simu, bidhaa nyingine zitakazotengenezwa ni pamoja na Tablet, Kompyuta mpakato, headphones pamoja na bidhaa za kielektroniki za majumbani pamoja na vipuri vyake.



Ungana Nasi Kwenye Mitandao ya Kijamii

KALIBU KWENYE GROUP NA PAGE YETU YA FACEBOOK KWA JINA LA ULIMWENGU WA TEKNOLOJIA.WHATSAPP KWA NAMBA 0653270429

 Ulimwengu wa teknolojia Sisi ni suluhisho lako namba moja katika masuala yote ya Teknolojia,ya TEHAMA TANZANIA tembelea Kila Siku.