FACEBOOK YAJA NA KIPENGELE KIPYA CHA MZIKI NA PICHA - ulimwengu wa teknolojia

Breaking

About Me

Peoples Solution

Monday 1 October 2018

FACEBOOK YAJA NA KIPENGELE KIPYA CHA MZIKI NA PICHA


facebook yaja na kipengele cha  kuchapisha picha/video ikiwa na muziki

Sote tunafahamu vyema kuhusu vitu ambavyo vinarushwa kwenye Facebook, vinaweza kuwa katika mfumo wa maandishi pekee au picha/picha jongefu pamoja na maelezo sasa imefahamika kuwa Facebook wapo njiani kuleta uwezo wa kuongeza muziki kwenye picha/picha mnato unayotaka kuichapicha.
Kwa lugha rahisi ni kile ambacho utakuwa umekirusha (picha/video) itakuwa na kuambatanisha na muziki ambao yule atayeona chapisho lako atakuwa na uwezo wa kubofya na kusikiliza.
Kitu hicho unaweza kuwa umeshakiona kwenye kipengele cha stories kwenye Facebook lakini sasa kinaletwa kwenye uso wa mbele (News Feed).

Utafanyaje kufanikiwa kuchapisha picha/video ikiwa na muziki?

Wakati umeshafanikiwa kuweka picha/picha mnato kutoka kwenye kifaa chako kwenda kwenye Facebook utabofya kwenye alama ya stickers kisha utabonyeza alama ya muziki kisha utachagua kipande cha muziki ambao utaupenda kurusha kwenye akaunti yako ya Facebook.

JE KWA MABADILIKO HAYA YANAYOTALAJIWA KUFANYIKA NA FACEBOOK UNADHANI NDIYO UTAKUWA  MWANZO WA KUIPOTEZA NA KUUPINGA MTANDAO WA INSTAGRAM

Ungana Nasi Kwenye Mitandao ya Kijamii

KALIBU KWENYE GROUP NA PAGE YETU YA FACEBOOK KWA JINA LA ULIMWENGU WA TEKNOLOJIA.WHATSAPP KWA NAMBA 0653270429

Machapisho ya picha