SIMU ZATUMIKA KUGUNDUA DALILI ZA KIFUA KIKUU(TB) - ulimwengu wa teknolojia

Breaking

About Me

Peoples Solution

Monday 1 October 2018

SIMU ZATUMIKA KUGUNDUA DALILI ZA KIFUA KIKUU(TB)

Teknolojia ya simu yatumika Tanzania kufanya uchunguzi binafsi wa ugonjwa wa kifua kikuu (TB).




Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt. Faustine Ngugulile.Amefanya uzinduzi wa huduma ya kifua kikuu kupitia teknolojia ya simu za mkononi unaojulikana kama “TAMBUA TB” Teknolojia hiyo imezinduliwa Septemba 21 mwaka 2018

Tukumbuke TB ni ugonjwa wa kuambukizwa  ambao unashika nafasi ya 9 dunia na  unaongoza kwa kuua watu wengi  ukitakunguliwa na ukimwi



Hadi sasa wahudumu 520 na 200 ambao ni wa kujitolea kutoka mikoa ya Dar es salaam ,Kilimanjaro,Geita,Mwanza,Arusha na Pwani.
HATUA ZA KUFUATA 
Huduma hiyo inayopatikana kwa njia ya simu bila malipo itampasa mtumiaji wa simu kupiga namba *152*05# BILA MALIPO ilikuweza kupata menyu ya “Afya na Ustawi wa Jamii” na kisha utabonyeza nambari sita (6) kufika kwenye kipengele kinachihusu kifua kikuu.

Itakubidi ufuate kila hatua na ujibu maswali kwa usahihi. Baada ya maswali kukamilika mfumo huo utakupa majibu kama una dalili za ugojwa wa kifua kikuu au hauna
Iwapo mteja atagundulika hana TB atashauriwa kujiunga na ujumbe mfupi wa simu wenye kutoa elimu ya kifua kikuu na aliyegunduliwa atasajiliwa kwenye mfumo wa mtoa huduma za afya.
Ungana Nasi Kwenye Mitandao ya Kijamii

KALIBU KWENYE GROUP NA PAGE YETU YA FACEBOOK KWA JINA LA ULIMWENGU WA TEKNOLOJIA.WHATSAPP KWA NAMBA 0653270429

 Ulimwengu wa teknolojia Sisi ni suluhisho lako namba moja katika masuala yote ya Teknolojia,ya TEHAMA TANZANIA tembelea Kila Siku.