KONGAMANO LA PILI LA TEHAMA TANZANIA LAFANYIKA MWEZI WA KUMI TAREHE 26 NA 27 - ulimwengu wa teknolojia

Breaking

About Me

Peoples Solution

Monday 1 October 2018

KONGAMANO LA PILI LA TEHAMA TANZANIA LAFANYIKA MWEZI WA KUMI TAREHE 26 NA 27

KONGAMANO LA PILI LA TEHAMA TANZANIA LAFANYIKA MWEZI WA  KUMI TAREHE 26 NA 27  UKUMBI WA MWL NYERERE.WATU WOTE MNAKALIBISHWA.

kongamano hilo limeandaliwa na Tume ya TEHAMA nchini .Ambalo litawahusisha wadau mbalimbali wa sekta ya teknolojia ya habari na mawasiliano kutoka ndani na nje ya Tanzania .
ICT (Information Communication and Technology) kwa Kiswahili TEHAMA ni sekta inayokua kwa kasi sana kwa sasa na inayoweza kusaidia ukuaji wa sekta zingine mbalimbali za uchumi.Kwa mara ya kwanza kongamano hilo lilifanyika mwaka 2017.hili linalofanyika sasa ni la pili kufanyika Tanzania
Kwa mwaka huu kongamano hilo litafanyika tarehe 26 na 27 mwezi wa kumi katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa mwl.J.K.nyerere.Ili ushiriki kongamano hilo itakulazimu ulipie laki tano ambazo itakubidi utangulize laki mbili kabla ya siku ya kongamano na utamalizia laki tatu baada ya kumalizika kwa kongamano.
Kongamano hilo linalojulikana kwa jina la( ANNUAL ICT PROFESSIONALS CONFERENCE) 2018 litawaleta kwa pamoja wadau mbalimbali waliokatika sekta hiyo hii ikiwa ni pamoja na;
  • Maafisa wa juu wa serikali, 
  • Mabingwa wa teknolojia za TEHEMA kutoka mashirika mbalimbali,
  • Wawikilishi kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali, wafadhili mbalimbali pamoja na makampuni ya kimataifa na ya nchini
  • Wasomi
  • Maafisa wa TEHEMA kutoka serikalini na sekta binafsi.
Ajenda kuu katika kongamano hilo ni pamoja na kuhimarisha mahusiana kati ya watalaam wa TEHAMA nchini Tanzania na wadau wengine wa TEHAMA nje ya Tanzania kwa lengo la kuifanya Tanzania kuzidi kuimarika katika sekta ya TEHAMA.

  • Kutoa mchango wa kimawazo utakaowezesha watu wenye fani ya TEHAMA kuweza kukuza vipato vyao na hatimae kukuza biashara zao. Wadau wenye uzoefu mkubwa kwenye TEHAMA watahusika kumfanya yule anayejishughulisha na masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kutokata tamaa.

  • Ufafanuzi mpana kuhusu makosa ya kwenye mtandao itakuwa ni moja ya mada katika kongamano hilo ambao maelezo ya kina yatatolewa kuhusu namna gani mdau/mtaalam wa masuala ya TEHAMA anaweza akaepuka na hatari ya kutumia vibaya mitandao ya kijamii, simu, n.k na hivyo kujikuta daima anaepukana na makosa ya matumizi mabaya ya teknolojia.

  • Matumizi ya programu tumishi, intaneti, namna ya kuboresha biashara kwa njia ya tehama ikiwemo matumizi ya mitandao ya kijamii, barua pepe na njia nyinginezo ni masuala yatakayojadiliwa kwenye kongamano hilo.

  • Matarajio ni kwamba kwa wale watakaohudhuria kongamano hilo ni kwamba mtu atatoka pale na mawazo mapana na mbinu mbalimbali zitazomuwezesha kuwa mmoja ya watu walobobea kwenye suala zima la TEHAMA.

    Ungana Nasi Kwenye Mitandao ya Kijamii

    KALIBU KWENYE GROUP NA PAGE YETU YA FACEBOOK KWA JINA LA ULIMWENGU WA TEKNOLOJIA.WHATSAPP KWA NAMBA 0653270429

    Ulimwengu wa teknolojia Sisi ni suluhisho lako namba moja katika masuala yote ya Teknolojia,ya TEHAMA TANZANIA tembelea Kila Siku.