SABABU ZA MWENYEKITI WA CHADEMA FREMAN MBOWE NA MBUNGE ESTHER MATIKO KUACHIWA HURU LEO KWA DHAMANA - ulimwengu wa teknolojia

Breaking

About Me

Peoples Solution

Thursday, 7 March 2019

SABABU ZA MWENYEKITI WA CHADEMA FREMAN MBOWE NA MBUNGE ESTHER MATIKO KUACHIWA HURU LEO KWA DHAMANA

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe na mbunge Esther Matiko wameachiwa kwa dhamana baada ya kushinda rufaa ya dhamana katika Mahakama kuu Dar es Salaam.
Mahakama Tanzania imetoa uamuzi leo katika kesi ya rufaa waliowasilisha viongozi wa upinzani Freeman Mbowe na Esther Matiko kupinga uamuzi wa hakimu wa kuwafutia dhamana katika kesi inayohusiana na maandamano dhidi ya serikali.
Freeman Mbowe, mwenyekiti wa chama cha upinzani, Chadema, na Esther Matiko, kiongozi wa chama hicho tawi la wanawake, wamekuwa kizuizini kwa kukiuka mashrati ya dhamana walioomba.
Walishutumiwa kwa kutofika mbele ya mahakama mara mbili walipotakiwa kwenda kukabiliwa na mashtaka dhidi yao, na kuchochea kufutiliwa mbali ombi la dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Novemba 23, mwaka jana.
Mbowe alijitetea kwa kusema alikuwa mgonjwa kwa mara zote alipotakiwa kufika mahakamani, huku naye Matiko alieleza kwamba alikosa kufika mahakamani mara moja kwasababu alikuwa kwenye kazi rasmi nchini Burundi.
Viongozi wa upinzani na makundi ya kutetea haki za binaadamu yamekuwa yakishinikiza kuachiwa kwao na kuwaita wafungwa wa kisiasa.
Wanaishutumu serikali ya rais Magufuli kwa kuwa ya kidikteta
Video ya wapinzani hao wawili wakiwasili katika mahakama kuu Dar es Salaam hapo jana Jumaano imesambazwa kwenye mitandao.