Hamia mtandao mwingine bila kubadili namba yako ya simu ya zamani - ulimwengu wa teknolojia

Breaking

About Me

Peoples Solution

Saturday, 23 June 2018

Hamia mtandao mwingine bila kubadili namba yako ya simu ya zamani

Je ungependa Kuhamia mtandao mwingine bila kubadili namba ya simu ya zamani

  
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania ‘TCRA’ kwa kushirikiana na watoa huduma za simu nchini wameanzisha huduma ambayo itamuwezesha mtumiaji wa simu kuhama kutoka mtandao mmoja wa simu kwenda mwingine bila kubadili namba, huduma hiyo imekwisha  kuanza March mosi Mwaka huu.
mambo 13 ya kufanya ili kuweza kufanikisha zoezi hilo

 hatua ya kwanza
ya kuhama mtandao mmoja wa simu kwenda mwingine kuwa ni kufika kituo cha mauzo au kwa wakala anayetambuliwa na mtoa huduma anakotaka kuhamia na kumueleza dhumuni lake.

Hatua ya pili
alisema Felician, ni kujaza fomu maalum ya maombi ya kuhamia mtandao aliotaka kuhamia.

 hatua ya tatu
 ni kujaza tamko la kukubali kuwa mteja anakubali kuwajibika kwa madeni yoyote ambayo yanatokana na huduma alizokuwa akipata kwa mtoa huduma wa awali kama yatakuwapo.

 hatua ya nne
 ni kuwasilisha kitambulisho chenye picha ambacho kinaweza kuwa cha taifa, kadi ya mpiga kura, leseni ya udereva, pasipoti au kitambulisho chochote rasmi kinachotambulika.

 pia mteja anatakiwa kuwa na simu ya kiganjani inayofanya kazi yenye namba inayotakiwa kubaki baada ya kuhama mtandao.

Hatua ya tano,
ni kuhamisha fedha zilizopo kwenye akaunti ya simu kabla ya kuhama ili kuepuka usumbufu.

hatua ya sita,
mwenye namba ya simu atatakiwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno wenye neno HAMA kwenda namba 15080 ambayo ni namba maalum ya kuhama.

hatua ya saba,
 mteja atapokea ujumbe mfupi wa maneno utakaomjulisha kuwa ombi lake limekubaliwa.

Hatua ya nane,
iwapo namba yako haikuzuiliwa au kusimamishwa kwa muda kutokana na kutokamilisha malipo ya madeni ya mtoa huduma wako wa awali, maombi yako yatashughulikiwa na utajulishwa kwa ujumbe mfupi wa maneno maendeleo ya mchakato huo,” alisema Felician.

KAMA KAWAIDA

Hatua ya tisa, mtoa huduma za simu za kiganjani atampatia mteja wake mpya laini mpya ya simu.

Hatua ya 10,
Ni kusitishwa kwa huduma za kifedha kwa muda mpaka namba ya mteja itakapohamishwa kwa mtoa huduma mpya. Kuanzia hapo mwenye namba atatumia huduma za kifedha za mtandao mpya kama huduma zipo

hatua ya 11,
 huduma za kupiga na kupokea simu na ujumbe mfupi wa maneno zitaendelea kama kawaida.

hatua ya 12,
mteja atakuwa amehama mtandao mmoja kwenda mwingine na kama patakuwa na ucheleweshaji, ni wa saa kadhaa, lakini ndani ya siku mbili pekee.

“Wakati huo namba yako ya zamani itakuwa imehamishwa kwa mtoa huduma wako mpya na laini yako ya awali haitatumika tena na utapokea ujumbe mfupi wa maneno kuwa uhamaji umekamilika,

hatua ya 13, mteja atatakiwa kuweka laini yake aliyopewa kwenye simu na endapo elimu zaidi itahitajika, mteja atatakiwa kwenda kwa mtoa huduma kujua namna ya kutumia huduma hiyo mpya.

MASHARTI NA VIGEZO

Mbali na kuelezea hatua hizo za kujiunga,  masharti na vigezo vitazingatiwa ambavyo ni mteja kutoweza kuhama na namba iliyofungiwa au kusitishiwa huduma kwa walipaji wa kabla ya huduma.

Mteja hataweza kuhama na salio lililopo na atatakiwa kutumia salio lake kwanza kabla ya kuhama kwani vinginevyo, litapotea.

Mteja hataweza kuhama iwapo ana mkopo kutoka kwa mtoa huduma wa awali, mikopo mingine kwa njia ya muda wa maongezi na pesa mtandao.

Mteja hataweza kuhama iwapo namba yake inahusishwa na uhalifu na imefungiwa.

Kwa wateja wanaotumia utaratibu wa malipo baada ya kutumia huduma, watatakiwa kulipa madeni ya matumizi yao kabla ya kuhama

Wateja hao, watatakiwa pia kukamilisha masharti ya mkataba ya mtoa huduma wake na kutizama masharti ya malipo kila mwezi kwa mujibu wa mkataba kabla ya kuhama

Alisema pia wataendelea kupokea ankara za matumizi hadi namba itakapohamishiwa kwa mtoa huduma mpya.

“Utaendelea kupokea ankara ya mwisho hadi siku 60 baada ya kuhamisha namba yako.

"Utapewa mpaka siku 30 za kulipa ankara hizo, vinginevyo utakuwa katika hatari ya uhamaji wako kusitishwa au namba yako kufungiwa.”

 ili kufahamu mtumiaji wa simu unayempigia amehama mtandao “utasikia milio miwili kabla ya simu kuita.

 kwa sasa kuna laini za simu milioni 40.1 nchini na kwamba lengo la kuleta huduma hiyo ni kuboresha na kupanua huduma za mawasiliano nchini.

ZINGATIA  HAYA

Ukihama kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine, kule ulikohamia unatakiwa ukae siku 30, baada ya siku 30 ndio unaruhusiwa kuhama.

Endapo utapiga simu kwenye namba ya mtu ambaye ameshahamia mtandao mwingine, utapata ishara ya milio miwili.

Huduma ya kuhama mtandao wa simu kwa namba ileile ipo nchi nyingi lakini ni kwa ajili ya nchi husika haivuki mipaka.

Kule unakohama haruhusiwi kuitoa namba ambayo umehama nayo, zikipita siku 90 haitumiki, ulikohamia watairudisha, Katika zoezi la kuhama.

zile huduma zote zinazohusiana na kifedha zitasimamishwa, kabla hujahama hakikisha fedha zako umezitoa.

Zoezi la kuhama mtandao ni bure ila mtoa huduma atalazimika kukupatia laini mpya, kukutoza fedha ya laini itategemea na mtoa huduma.

                                 Ungana Nasi Kwenye Mitandao ya Kijamii 
                                              Ulimwengu wa teknolojia  
Sisi ni suluhisho lako  namba moja katika masuala yote ya Teknohama, Tembelea Kila Siku.