Jeshi la Polisi nchini kupitia kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), kwa kushirikiana na Government e-Payment Gateway (GePG), limeanzisha mfumo wa upatikanaji wa fomu ya upotevu (Police Loss Report), kupitia mtandao wa https://Lormis.tpf.go.tz na kufanya malipo kwa njia ya simu kwa mfumo wa GePG.
Mfumo huo ulianzishwa mwezi Machi, 2019 na kitengo cha TEHAMA Makao Makuu ya Polisi, kwa lengo la kupunguza gharama na kurahisisha upatikanaji wake katika vituo vya Polisi, kwa sasa mfumo unafanya kzi nchi nzima humuwezesha mtu yeyote kufanya maombi na malipo ya Loss Report kwa njia ya mtandao na baadaye mwombaji kwenda Kituo cha Polisi ili kukamilisha huduma hiyo.
kama umepoteza kitu na unaitaji loss report form (fomu ya taarifa ya kupotelewa kitu) ya police tembelea tovutihttps://lormis.tpf.go.tz/
Mwombaji wa fomu ya upotevu kwa njia ya mtandao, atatakiwa kufuata hatua zifuatazo:-
HATUA MUHIMU
1. Jaza hiyo form kupitia mtandao kwa kutoa maelezo ya upotevu.
Akisha jaza fomu hiyo atapatiwa ‘control number’.
2. Utapata Control Number 99XXXXXXXXXX
Baada ya kupatiwa ‘control’ namba atalipia Tsh 500/= kwa njia ya mtandao.
3. Lipa Tsh 500/= kwa njia ya mtandao
4. Nenda kituo chochote cha polisi kwa ajili ya uthibitisho
Baada ya kufanya malipo atatakiwa kwenda kituo chochote cha Polisi kwa ajili ya uthibitisho.
5. Print barua yako kwa wakati wako.
Baada ya kukamilisha hatua zote mwombaji ataprinti fomu hiyo kwa wakati wake.
Jeshi la Polisi nchini linatoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano katika mapambano dhidi ya uhalifu kwa kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu ili kuendelea kudumisha amani na usalama wa nchi.
Tafadhari tuwajulishe wananchi kila tunapopata fursa ya kukutana nao awe mmoja au wengi.
LIPIA BARUA YA UPOTEVU (LOST REPORT) KUPITIA SIMU YAKO
Mfumo huo wa malipo unafanya kazi kwa kutumia kamera ya simu janja ambayo inaskani msimbo (CODE) na kisha kukamilisha malipo ndani ya muda mfupi.
Baadhi ya Watanzania wameziomba kampuni kama Visa na Mastercard kutoa elimu zaidi kwa umma kwa kuwa huduma hiyo ni nzuri lakini bado haitambuliki na watu wengi.
Huduma hii huenda ikaondoa kabisa haja ya mtu kutembea na fedha kwani huduma nyingi muhimu zimefikiwa nayo. Maduka makubwa, sheli na hata migahawa.
Ni ukweli usiopingika kuwa teknolojia ya msimbomilia imerahisisha uwezo wa kufanya miamala ndani ya muda mfupi na hasa ukizingatia watu wenye simu janja inazidi kuongezeka mwaka haaadi mwaka nchini Tanzania.
Katika dunia ya leo wengi wetu tunatumia simu janja katika kufanya mambo mengi tu lakini mambo yalivyo hivi sasa mfumo wa QR Code unasaidia kurahisisha miamala duniani kote lakini hata kwa Tanzania.
Dar es Salaam. Kwa kila mtanzania anayefanya manunuzi kwa kutumia teknolojia ya simu janja, neno “QR code” sio kitu kigeni kwa kuwa limekuwa likisika kila kukicha.
Kampuni nyingi zimekuwa zikitumia neno hilo katika kuhamasisha matumizi ya teknolojia mpya ya kufanya malipo baada ya kununua bidhaa au huduma.
Mfumo huo wa malipo unafanya kazi kwa kutumia kamera ya simu janja ambayo ina skani msimbo (CODE) na kisha kukamilisha malipo ndani ya muda mfupi.
Ili kuendeleza ushindani, kampuni kubwa duniani na nyumbani zinazotoa huduma ya kufanikisha malipo zimejitahidi kubuni njia mbadala ili kutoa huduma bora lakini kubaki katika soko kutokana na kukua kwa teknolojia.
Katika ubunifu huo, kampuni hizo zimekuwa zikishirikiana na taasisi za huduma za kifedha kama benki na kampuni za simu zinazotoa huduma za kifedha ili kufanikisha miamala ya manunuzi kupitia teknolojia hiyo ya kulipa kwa QR Code.
Hivi karibuni kampuni ya kimataifa ya Visa yenye makao makuu yake nchini Marekani inayojihusisha na huduma za kifedha ilizindua huduma ya kuskani QR Code hapa nchini Machi 12, 2019 ili kurahisisha malipo ya huduma na bidhaa mbalimbali.
Visa imeungana na taasisi 15 zinazotoa huduma za kifedha zikiwemo benki za CRDB, NBC, NMB, na kampuni ya simu ya Halotel kumpa mteja mawanda mapana zaidi ya kuchagua namna ya kulipa. Kwa sasa, huduma hiyo inapatikana katika sheli na maduka ya jumla ya watoa huduma zaidi ya 2,000.
Mteja anaweza kuskani QR Code kwa kutumia simu janja na kulipia bidhaa na huduma kirahisi
Kuna teknolojia nyingi za malipo zinaendelea kubuniwa duniani, je mfumo huu wa malipo wa QR Code una maana gani kwa wateja na watoa huduma?
Wafanyabiashara ambao sio tu wametumia mfumo huo wa Visa bali hata mingine ambayo ilikuwepo awali wamesema mfumo mpya wa kampuni hiyo una kasi kuliko njia ya kadi na hata ile ya kulipa kwa waleti za mitandao ya simu.
Meneja Mkuu wa maduka ya Shoppers, Mahesh Venkatesh amesema imepunguza foleni ya malipo kwa wateja wake wanaotumia malipo ya kadi kwa kuwa ilikuwa inachukua muda mrefu kukamilisha malipo ya mtu mmoja hapo awali.
“Kama mtu mmoja anakaa kwenye foleni kwa dakika 5, inaweza kusababisha mtu kuahirisha kufanya manunuzi kama ana haraka lakini kwa mfumo huu wa QR Code mtu analipa kwa dakika 2 tu. Inarahisisha uharaka wa kutoa huduma na zaidi inaongeza mauzo,” amesema Venkatesh.
Mbali na kupunguza foleni, watumiaji wa mfumo huu wanaeleza kuwa unaondoa usumbufu wa kutafuta chenji ambayo mara kadhaa husababisha baadhi ya wauzaji wasio wavumilivu kuahirisha mauzo.
Maduka mengi jijini Dar es Salaam sasa yamefikiwa na huduma ya QR ya kampuni ya Visa kuwarahisishia wateja wao kufanya malipo ya bidhaa.
Sambamba na hayo, miaka ya zamani kulikua na matukio mengi ya uvamizi kwenye maduka au sheli mbalimbali jijini Dar es salaam na uvamizi huo ulilenga kupora pesa kwenye vituo vya mafuta. Kupitia mfumo wa QR,
“Inaondoa changamoto za usafirishaji wa fedha baada ya mauzo ya siku nzima kwa sababu baada ya malipo pesa inaingia moja kwa moja kwenye akaunti ya mtoa huduma. Pia inaondoa uwezekano wa kuibiwa kwa sababu ya kutembea na maburungutu ya pesa,” amesema Mohamed Omar Meneja wa kituo cha mafuta cha Puma, Upanga jijini Dar es Salaam.
Pamoja na uzuri wa teknolojia hiyo bado elimu haijawafikia watu wengi katika kubadilisha mfumo wa malipo kutoka kwenye fedha taslimu kwenda kwenye malipo mtandao.
Baadhi ya Watanzania ambao wameweza kutumia huduma hiyo wameziomba kampuni kama Visa na Mastercard kutoa elimu zaidi kwa umma kwa kuwa huduma hiyo ni nzuri lakini bado haitambuliki na watu wengi.
"Asilimia kubwa ya watanzania hawatumii huduma ya kadi wakijua njia za kulipia huduma kwa simu zinarahisisha malipo. Elimu itolewe kwani huduma hii ni nzuri,"
Baadhi ya huduma za aina hii mara nyingi huwa kuna makato pale mteja anapolipia huduma yoyote kwa kulingana na kiasi anacho kitumia.
faida ya huduma pamoja na changamoto zake
alijaribu mara tatu kununua bidhaa kupitia mfumo wa malipo ya QR Code chini ya Visa na kubaini kuwa hakuwa amekatwa kutokana na miamala aliyokuwa amefanya katika kununua bidhaa hizo.
Pamoja na uzuri wa teknolojia hiyo bado elimu haijawafikia watu wengi katika kubadilisha mfumo wa malipo kutoka kwenye fedha taslimu kwenda kwenye malipo mtandao.
Kupitia mfumo huo hakuna haja tena ya kuhamisha fedha kutoka benki kwenda kwenye akaunti za mitandao ya simu ili kufanya malipo. Mteja atalipa moja kwa moja bila makato kutoka benki au mtandao wake wa simu kama Tigo Pesa au M-Pesa bila uwepo wa dalali.
“Ukilipa shilingi elfu tano, ni elfu tano tuu itakayokatwa. Hakuna ada ya malipo anayotozwa mtejahuduma nyingi muhimu zimefikiwa nayo. Maduka makubwa, sheli na hata migahawa.
Kupitia malipo ya QR, muuzaji anauwezo wa kuongeza mauzo na hata kupata wateja ambao ni waaminifu kwani imetoa uwanda mpana zaidi wa kulipia manunuzi na huduma.
Weka simu yako ya smartphone kuwa katika muomekano wa kompyuta.
kweli ni kwamba siku hizi watu wengi hutumia simu zenye nguvu pengine kuliko hata baadhi ya kompyuta hasa za zamani, kutokana na sababu hiyo pengine ulishawahi kuwaza kutumia simu yako kama kompyuta au PC. Sasa mwaka huu 2019 hii sio ndoto tena kwani sasa utaweza kutumia simu yako ya Android kama kompyuta kwa asilimia 100
Kuwezesha hilo kampuni ya Jide Technology imefanikiwa kutengeneza programu ya Remix OS for Mobile programu ambayo itakuwezesha kutumia simu yako kama kompyuta kwa kuichomeka tu kwenye kioo cha kompyuta yako.
Akizungumza na mhariri wa tovuti ya Theverge kiongozi wa kampuni hiyo alisema kuwa mteja atahitaji install sehemu ya programu hiyo kwenye simu yake pamoja na kuweka programu ya Google Play kisha baaada ya hapo pale mtumiaji atakapo chomeka simu yake kwenye kioo cha kompyuta programu hiyo humpa muonekano bora pamoja na uwezo wa kutumia keyboard pamoja na mouse kwenye kioo hicho. Hii sio mara ya kwanza kwa kampuni za teknolojia kubadilisha simu kuwa kompyuta, kwani hata kampuni ya Microsoft nayo iko mbioni kutoa programu nzima ya Windows 10 kwaajili ya simu za mkononi au smartphone.
Kwa sasa programu ya Remix OS iko kwenye hatua za mwisho hivyo hivi karibuni jiandae kuitumia kwanye simu yako na ubadilishe smartphone yako kuwa kompyuta.
Habari ndugu wasomaji wa ulimwengu wa teknolojia.siku ya leo TUmekuja hapa kujuzana kuhusu kumiliki blog yako mwenyewe.
najua wengi mmekuwa mkijiuliza ni namna gani unaweza kutumia blog kama chanzo cha mapato.Ni kumiliki blog mwanzoni ni kazi ngumu inayoitaji utayali wa mali,akili na muda wako.swala la kutengeneza blog ni rahisi na inaweza kukuchukua masaa kadhaa kukamilika.
ANGALIZO
Ili uwanze kuingiza hela kupitia blog inahitaji juhudi zako mwenyewe.pia kuna hatua chache za kufata ili kuanza kulipwa.sisi kwa leo tutaongelea hatua za kufuata ili umiliki blog yako. kuhusu kuingiza kipato tutazunguza katika mada zijazo .
HATUA ZA KUTENGENEZA BLOG
zipo njia nyingi za kukuwezesha kumiliki blog yako bure bila kulipia nitakutajia chache
kama blogger.comwordpess.comweebly.comwebs.comna kuna nyingine nyingi lakini sisi leo tuangazie kufungua kutumia blogger unachotakiwa kufanya ni kutembelea link yao ambayo ni
hiiwww.blogger.comitakuletea muonekano huu Hapo unachotakiwa kufanya kama unamilliki email ya gmail ingiza hapo na nywila (password) yako kama huna utafungua akaunti mpya kwa kubofya maneno yanayo someka fungua akaunti mpya (creat new account) watakuletea fomu yao utajaza na kukubaliana nao kisha watakupatia akaunti yako sasa utakuwa umesha sign in utaona muonekano huu
kwasababu ndio mara ya kwanza muhimu kuna sehemu ya lugha kwa faida yako badili uweke kiingereza cha kingdom hii itakusaidia kupata nafasi ya kujisjili na matangazo ya ADSENSE, Kama unahitaji msomaji wako aje kuona jina lako kamili kwenye machapisho (post) yako jina lako kamili bofya hapo kwenye google+ profile.kama huhitaji bofya hapo kwenye creat a limited blogger profilesisi tunahitaji jina kamili tutabofya kwenye google+ profile. Tutabofya hapo kwenye creat profile hapo tutakubaliana na masharti yao mpaka mwisho tutakapo kutana na neno finish utabofya neno hili kama watakupeleka kwenye profile yako ya google+ achana nayo tembelea link yao ya www.blogger.com kutokana tulishamaliza kukubaliana nao sasa Utabofya hapo kwenye neno continue to blogger Hapo utabofya kwenye neno new blogneno hili linapatikana upande wa kushoto utabofya neno hilo
Hapo utajaza kicha cha blog kwenye Title na adress ya blog ambayo unahitaji usiandike hili neno .blogspot.com huwa linakuja lenyewe kisha chagua template inayokuvutia kisha bofya neno creat blog mpaka kufikia hapo utakuwa umeshakamilisha kumiliki blog yako
hapo kazi ni kwako kuchapisha tu na kusubiri neema ya mungu ya kupata adsense na wasomaji wengi ili uweze kunufaika kwa kupitia blog yako kama kuna kitu kitakusumbua kuhusu kufungua blog weka coment hapa chini nitakusaidia
Habari zenu tena ndugu zangu katika dunia hii ya teknolojia . leo tutakumbushana/kujifunza njia Rahisi ya kuweka/kutumia app za simu janja(smartphone) kwenye computer zetu ambazo tumezoea kuziona kwenye playstore. Ni kweli tunatamani sana kutumia baadhi ya aplication za simu kwenye computer zetu lakini hatujui tufanyeje ili zikae na tuzitumie hizo mobile app kwenye laptop zetu. ulimwengu wa teknolojia tupo kwa ajili yako na tunahakikisha upitwi na kitu kwenye teknolojia,leo tutakujuza njia rahisi na nyepesi za kuweka application za simu yako kwenye computer yako.Nakusihi fuatana nami ili upate kunufaika na hili fuata haya upate kufurahia mashine yako bila kukosa chochote Pakua programu inayoitwa Bluestacks ni bure ipakue (download) hapa http://www.bluestacks.com/download.html
Kisha Install ni bure yaani offline sasa, Ukimaliza itakuletea muonekano huu
Chagua lugha mimi ningechagua kiingereza sababu hakuna kiswahili
endelea next step zote kisha itakuomba uweke email au ufungue emal mpya kama hauna. kama unayo weka email yako.Ita load kisha itafunguka
mpaka hapo utakuwa umesha kamilisha sasa unaweza kutafuta program unayotaka na kuipakua kama play store
Kuna matumizi mengi sana ya kamera ya simu janja zetu ukiachana na yale tuliyo yazoea ya kupiga picha tu
Unajua kama kamera ya simu janja yako inaweza ikawa na matumizi lukuki ambayo kwa namna moja au nyingine yanaweza kurahisisha maisha yako
1. Scan Nyaraka
Kamera ya simu janja yako pia inaweza ikawa ina’scan’ nyaraka tofauti tofauti. Pata picha unakuwa na ‘scanner’ ambayo ipo mfukoni kwako. Unaweza uka ‘scan’ vitu kama vile mikataba,risiti au kitu chochote kilichopo katika karatasi na unataka ukifanye kiwe kidigitali
Baada ya hapo unaweza ukaamua kutuma vitu hivyo katika barua pepe au unaweza ukavihifadhi katika mfumo wa PDF au JPG Unataka ku’scan’ vitu?
Kwa iOS shusha(download) Evernote
Kwa Android shusha Google Drive ndani yake kuna kipengele cha ku’Scan’
2. Tumia Kamera Ya Simu Janja Yako Kama Mkalimani Wako
Teknolojia inabadilisha dunia kwa kiasi kikubwa sana miaka kadhaa iliyopita ningebisha kata kata kama jambo hili lingeweza kutokea. Hivi unajua unaweza ukatumia kamera ya simu yako ili kutafsiri lugha Fulani?
Kumbuka kuna maandishi huwa yanaandikwa na mara nyingi tunakuwa hatuyaelewi kwa mfano ukiwa katika mgahawa ikaja menyu yenye maandishi ya kigeni hapo ndipo huduma hii utakapo ona ubora wake
Ukiwa na App ya Google Translate, ambayo inaweza kutafsiri lugha 29 utafanikisha hilo kwa kuweka kamera mbele ya maandishi yaliyoandikwa na hapo App itafanya zoezi zima la kutafsiri kwenda katika lugha unayotaka
3. Tumia Kama Kamera Ya Ulinzi
Hivi ulishawahi kuwa na hamu ya kutumia kamera ya simu yako kama njia ya ulinzi? Labda una kamzigo kako pale ndani na unataka ukachunge. Ondoa shaka kuna App maalum ambazo zinakuwezesha kufanya hayo yote. App hizi hutumia kamera ya simu janja ili kugundua mwondoko wa aina yeyote (motion) na kisha kukutaariffu kupitia barua pepe (e-mail) yako
Kwa Android shusha App ya Silent Eye
4. Fuatilia Barcodes Za UPC
Wakati mwingine wakati ukiwa unafanya manunuzi ya vitu na ukawa huna uhakika kama unanunua vitu imara achana na ku Google, tumia kamera ya simu janja yako kuweza kuichunguza bidhaa hiyo.
Zile App ambazo zinamsaidia mtu ku’scan code’ za UPC zinampatia mtu taarifa za bidhaa katika kiganja chake kabisa. Ukiachana na taarifa kuhusiana na bidhaa bado utaweza kufananisha bei tofauti tofauti ya bidhaa hizo ili kujua kama umepewa bei nzuri au la
Kwa Android shusha App ya ShopSavvy Barcode and QR Scanner
5. Shangaa Anga
Hivi ushawahi kukaa usiku na ukawa unashangaa anga na ukaanza kujiuliza maswali kama baadhi ya vitu unavyoviona ni nyota au ni sayari zingine? Sasa App ya Skyview kwa Android na iOs itakupa majibu yote
App hii inatumia kamera ya simu yako katika kukuonyesha jinsi anga ilivyo cha kufanya hapa wewe elekeza kamera ya simu janja yako katika anga.
Pia kama remote ya Tv au kisimbusi inasumbua unaweza kutumia kamera ya simu kuona kama remote hiyo inatoa mionzi au la kabla ya kuchukua hatua nyingine kama kubadili betri au kuitengeneza.Washa kamera ya simu,nyoshea kile kitaa cha remote kwenye kamera huku ukiwa una bonyeza vitufe kwenye remote.Utaona mwanga unawaka kwenye screen ya simu endapo kama remote ni nzima